Moto mkubwa uliotokozea wakati wa jioni umeteketeza kabisa moja kati ya nyumba mbili za mfanyabiashara maarufu wa Zanzibar Naushad Mohamed na kusababisha hasara ya mamilioni ya fedha.


Moto huo uliutokozea eneo la Beitras Njekidogo ya mjini Zanzibar ulianza wakati wa saa kumi jioni lakini pamoja na kikosi cha zimamoto kufika kwa mudamfupi upepo mkali uliokuwa ukivuma ulisababisha moto huo kuwa na kasi na kuweza kutekekteza nyumba hiyo huku taarifa ya familia ikielezea chanzo cha moto huo umetokana na hitilafu ya umeme.
Wakizungumza na ITV mmiliki wa nyumba hiyo Bw Naushand Mohamed mohamec amesema moto huo ulikuja ghafla na yeye alikuwa katika nyumba nyingine huku aksiema moto huo umeangamiza hati zake zote za nyumba na nyingine za biashara huku mkuu wa opresheni wa kikosi cha zima moto sasa wa zimamoto Suleiman amesema moto huo ulikuwa mkubwa.
Moto huo ulizua mtafaruku mkubwa huku umati wa watu kujazana nje ya jengo hali iliyosababisha jeshi la polisi kuweka ulinzi mkubwa ambapo polisi walilazimika kulinda nyumba hiyo ndani na nje wakiwa na silaha.
Share To:
Magpress

MagPress

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

0 comments so far,add yours