Serikali imesema matukio ya ugaidi na uharamia yanayoendelea katika ukanda wa Afrika ni changamoto kubwa katika nchi kwa sasa hivyo kunahitajika jitihada za maksudi katika kukabilina na matukio hayo.
Waziri wa nchi ofisi ya rais serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Mh.Haji Omar Kheir ameyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya awali ya askari polisi na uhamiaji katika chuo cha taaluma ya polisi Moshi.
 
Amesema katika kukabiliana na matukio hayo askari polisi hapa nchini hawana budi kuimarisha mahusiano mazuri na wananch sanjari na kufanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia misingi ya haki za binadamu ili iwe rahisi kupata taarifa za wahalifu wa matukio hayo ambayo yanahatarisha amani.
 
Kwa upande wake mkuu wa jeshi la polisi nchini Igp Ernest Mangu amesema pamoja na takwimu za mwaka 2014  za kupima viwango vya uhalifu na usalama duniani kuonyesha Tanzania ni nchi ya kwanza katika ukanda wa afrika mashariki na kusini mwa afrika kuwa salama, bado kuna matishio kadhaa ambayo yameanza kujitokeza na  kuhatarisha amani na usalama katika nchini. 
 
Naye mkuu wa chuo cha taaluma ya polisi moshi (MPA) afande Matanga Mbushi amesema jumla ya askari polisi na uhamiaji 3210 wamehitimu mafunzo hayo na wengine 299 waliachishwa mafunzo hayo kutokana na utovu wa nidhamu ikiwemo kugushi vyeti kwa ajili ya kujiunga na jeshi hilo.
 
Katika hafla hiyo pia askari hao wameonyesha umahiri na ukakamavu wa hali ya juu katika kukabilina na wahalifu kwa kuonyesha mazoezi ya vikwazo. 
 

Share To:
Magpress

MagPress

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

0 comments so far,add yours