Jeshi la Polisi la mkoa wa Morogoro limekamata magunia matano ya bangi yalikuwa yamefungwa katika fuso iliosheheni samaki wabichi wakitokea Mwanza kuelekea jijini Dar es salaam.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Lenard Paul amesema askari wa jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarni walitilia shaka gari hilo eneo la Kingulwira mjini Morogoro ambapo alikagua na kubaini magunia matano ya bangi yakiwa yamefungwa katikati ya samaki wabichi na watuhumiwa watatu akiwemo dereva tigo na mwenye mzigo wa bangi wanashikiliwa na jeshi la polisi.
 
Nao watuhumiwa wa tukio hilo walipohojiwa wamekiri kuwa ugumu wa maisha ndio sababu inayowapelekea kuingia kwenye biashara ya bangi.
Share To:
Magpress

MagPress

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

0 comments so far,add yours