Mmoja kati ya wafanyabiashara wakubwa wa nchini Marekani mwenye asili ya Afrika Dr.Robert Shumake amekubali kuzileta treni za kisasa katika jiji la Dar es salaam ili kusaidia kutatua kero ya usafiri katika jiji hilo ambapo anatarajia kutumia zaidi ya shilingi Bilioni arobaini kufanikisha hilo muda wowote kuanzia sasa.
Akizungumza mara baada ya kutia saini makubaliano ya uletaji wa treni hizo Dr.Shumake amesema anatarajia treni hizo zitafanya kazi saa ishirini na nne na anaisubiri serikali ya Tanzania imalize tathmini ya gharama za mradi huo na yeye aweze kutoa fedha za kuufanikisha.
 
Naye waziri wa uchukuzi Dr.Harrison Mwakyembe amesema treni hizo zitafanya kazi kati ya Stesheni na Pugu na zitatumia miundombinu ya reli iliyopo ila kutakuwa na ujenzi wa reli zingine katika baadhi ya sehemu kuruhusu treni kupishana.
 
Share To:
Magpress

MagPress

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

0 comments so far,add yours