Wabunge Bila ya kujali itikadi za vyama vyao wamelitaka Bunge kuachana na Barua ya mahakama inayotaka kuzuia sakata la Kashfa ya fedha katika akaunti ya Tegeta ESCROW lisijadiliwe na kutolewa maamuzi Bungeni kwa kuwa liko Mahakamani.
Wakitoa ushauri kwa Bunge na kamati ya uongozi, Mbunge wa kigoma kusini Mhe.Davidi Kafulila amesema mahakama imekosa uhalali mamlaka ya kisheria na kikanuni  ya kuzuia Bunge kuendelea na utaratibu wake katika kufuatilia sakata la ESCROW. 
 
Baadhi ya wabunge kutoka chama tawala CCM wamelitaka Bunge kuchukua hatua kataka hilo kwa kuhakikisha taarifa ya kamati ya Bunge ya Hesabu za serikali kuhusu wizi huo wa mabilioni ya fedha iwasilishwe bungeni.
 
Kwa upande wao wabunge wa chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA wametaka Barua hiyo kuwekwa mezani ili kuliwezesha Bunge kumjadili kiongozi wa mahakama kama hoja mahususi kwa mujibu wa kanuni ya 64 1e ambaye amediriki kuingilia mamlaka ya Bunge na kulifundisha kazi zake. 
 
Akielezea  kwa ufupi hatua ya kamati ya PAC inayochunguza sakata la ESCRO ilipofikia mwenyekiti wa kamati ya PAC amependekeza kuwepo kwa mjadala ili kuweza kuondoa Minong’ono pamoja na kuwachukulia hatua wahusika kwa mujibu wa sheria. 
Aidha akizungumzia sakata hilo,waziri mkuu mheshimiwa mizengo pinda amependekeza katika kutatua sakata hilo ni lazima Bunge litumie Busara kubwa ili kuahikikisha maamuzi yatakayotolewa hayataleta hisisa za muingiliano wa majuku na mahakama.

Share To:
Magpress

MagPress

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

0 comments so far,add yours