Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dr Ali Mohamed Shein amewataka watendaji serikalini kujali nchi na sio maslahi yao na kuwakemea wale wanaofananisha serikali sawa na makampuni yao.
Dr Shein ametoa tahadhari hiyo hapa Zanzibar wakati akiufunga mkuatno wa nane wa baraza la biashara la Zanzibar ambapo amemsema ni jambo la kushnagaza kuona baadhi yawatendaji wamekuwa wakijali maslahi yao na kuidharau seriklai amesema serikali imepania kuleta mabadiliko ya uchumi kwa kushirikiana na sekta binafsi.
 
Mapema balozi seif Ali Idi makamu wa pili wa rais ambaye ndie mtendaji mkuu wa seriklai amekiri kuwepo kwa urasimu wa watendaji katika kupitisha miradi yauwekezaji hali ambayo inaiharibia jina la Zanzibar ambapo baadhi ya taarifa zinazosambazwa zinatangaza vibaya Zanzibar juu ya uwekezaji.
 
Hata hivyo waziri wa biashra, viwanda na masoko Mhe Nassor Ahmed Mazuri akitoa tathmini ya biashara amemsmea pamekuwepo na ongezeko kubwa la biashara za nje nakwaupande wa bishara ya ndani pande mbili za muungnao zimepata mafanikoi makubwa ya biashara.
 
Mkutano huo wa nane ambayo mwenyekiti wake ni rais wa Zanzibar unawakutanisha watendaji wote wa seriklai na wafanyabiashara wasekta binafsi.
Share To:
Magpress

MagPress

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

0 comments so far,add yours