Chama cha demokrasia wilayani Iringa kimelalamikia rafu na kasoro mbalimbali zilizojitokeza katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Disemba 14 nakusema kuwa uchaguzi huo uligubikwa na kasoro nyingi ambapo wakati uchaguzi huo ukiendelea hii leo watu wasiojulikana wamemshambulia kwa nondo na mapanga katibu wa mbunge wa Iringa mjini Bwana Joseph Mgima.
Akizungumza kwenye mahojiano na ITV Bwana Mgima amesema tukio hilo lilitokea usiku wa jana majira ya saa mbili usiku wakati alipokuwa akienda kuzungumza na mawakala wa chama chake kwenye mtaa wa Bwawani kata ya Mkwawa ndipo alipokutana na watu hao waliokuwa kwenye bajaji mbili ambapo mmoja wa watu hao alimpiga teke na kuangukia mtaroni ndipo watu wengine sita kutoka kwenye hizo bajaji walipoanza kumpiga kwa mapanga.
 
Mwenyekiti wa baraza la vijana la chaama cha demokrasia na maendeleo Chadema wilaya ya Iringa Leonce Marto amesema tukio hilo linauhusiano mkubwa na uchaguzi wa marudio wa wenye viti na wajumbe katika mitaa 19 katika manispaa ya Iringa akiwatuhumu wapinzani wao wa CCM kutumia mbinu chafu kushinda kwenye mitaa hiyo huku kamanda wa polisi mkoani Iringa Ramadhani Mungi akisema jeshi hilo linachunguza tukio hilo na litawashughulikia wote watakaobainika kufanya uhalifu huo.
 
Zoezi la uchaguzi linafanyika hii leo ikiwa ni marudio baada ya baadhi ya maeneo katika mitaa ya manispaa ya Iringa kushindwa kufanya uchaguzi huo kutokana na kasoro mbalimbali zilizojitokeza ikiwemo kukosekana kwa baadhi ya vifaa ambapo jumla ya mitaa 10 inarudia kuchagua wenyeviti wa mitaa na wajumbe wao na mitaa mingine 9 inarudia uchaguzi wa wajumbe baada ya wajumbe hao kugona kwa idadi ya kura.

Share To:
Magpress

MagPress

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

0 comments so far,add yours