Kiongozi wa kanisa katoliki nchini Mwadhama Polycarp  Kadinali  Pengo  amewataka wakristo kote nchni kumuomba mungu aliepushe taifa na  matukio ya ubaguzi, vita, ugaidi  na mauaji yanayotokea Duniani ikiwemo mauaji ya kikatili ya wanafunzi waumini wa kikristo yaliyotokea katika  chuo kikuu cha Garisa nchini Kenya.
Akizungumza katika ibada ya Jumatatu ya Pasaka iliyohudhuriwa na mamia ya wanachama wa shirikisho la kwaya katoliki nchni, Kadinali Pengo pia amewataka wakristo nchini kumuomba mungu asafishe hali iliyojitokeza nchini Kenya na kuwataka kuwawajasiri na kubaki katika misimamo ya imaniya  kikristo kwa kutamka ukweli  iwapo hali hiyo italazika kujitokeza.
 
Aidha kuhusu katiba inayopendekezwa,Padinali Pengo  amesema kama kiongozi wa  Dini hawezi kurudia au kubadilisha kauli aliyokwisha itoa kwa wananchi,kwani kufanya hivyo kutaweza kusababisha ugomvi ambapo amewataka waumini wa kanisa katoliki kusambaza kauli hiyo kote nchni.
 
 Awali kiongozi wa kanisa katoliki nchini Mwadhama Polycarp  Kadinali  Pengo ametaka wananchi waachiwe wasome katiba inayopendekezwa na kufanya maamuzi wenyewe.
Share To:
Magpress

MagPress

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

0 comments so far,add yours