Wananchi wa kata ya Nyankende katika wilaya ya kahama mkoani Shinyanga wameitaka serikali kutafuta mbinu za kupandisha bei ya pamba zao ambalo linategemewa katika shughuli zote za kimaendeleo hali  inayotishia kuporomoka kwa uchumi katika mkoa wa shinyanga na kuwafanya wananchi kuishi maisha duni na ya dhiki.
Hayo yamesemwa na diwani wa kata ya Nyankende wilayani kahama Mh. Doa Limbu kwa niaba ya wananchi wa kata hiyo katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na mkuu wa mkoa wa shinyanga ili kujadili changamoto zinazowakabili wananchi hao ambapo kata hiyo haijawahi kutembelewa na mkuu wa mkoa yeyote tangu ianzishwe.
 
Naye mkuu wa wilaya ya kahama Bw.Benson Mwampesya amewataka wananchi wa kata ya Nyankende kulima mazao mengine ya biashara na chakula ikiwemo zao la alizeti kwakuwa kuanguka kwa bei ya zao la pamba sio swala la tanzania pekee na hakuna namna ya kupandisha bei ya zao hilo kwa haraka.
 
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa shinyanga Bw.Ally Nasoro Rufunga amewaahidi wananchi hao kuwaletea wawekezaji watakaoingia ubia katika kilimo cha mkataba hali itakayosababisha kukua kwa sekta ya kilimo katika kata hiyo.
Share To:
Magpress

MagPress

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

0 comments so far,add yours