Mashirika mbalimbali na watanzania kwa pamoja wameombwa kuwa na utamaduni wa kuchangia  na kuboresha shule maalumu ambazo zina walemavu wa ngozi ,badala ya kusubiri matukio ya uvamizi kutokea na kuanza kuchukuwa hatu ,kwa kufanya hivyo kuta saidia walemavu  wa ngozi kupata elimu bila ya kuwa na wasiwasi ya kuvamiwa na baadhi ya watu wenye nia mbaya.
Mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Parseko Vicent Kone amesema hayo katika hotuba yake iliyo somwa na mkuu wa wilaya ya Singida, Bwana  Said Amanzi katika  hafla ya kukabidhi mradi wa uboreshaji wa miundombinu rafiki kutoka shirika la Koica la nchini korea,na kusema kuwa mashirika kutoka  mataifa  mengine wame weza kuchangia na sisi watanzania   inatubidi kuchangia kwani jukumu la kuwalinda walemavu wangozi ni ni la watanzai wenyewe na kuhakikisha wana pata  ulinzi na elimu kama watu wengine.
 
Kwa upande wake  meneja mradi wa kujitolea kutoka shirika la Koica nchini korea  Bi. Park Jieun amesema mradi wa uboreshaji  wa miundombinu katika chuo cha ufundi na marekebisho kwa watu wenye ulemavu sabasaba umegarimu zaidi ya shilingi milioni arobaini na mbili kwa ajili ya kuboresha mazingira ya chuo kwa kujenga mabweni,matanki ya maji na kuwasaidi walemavu  ili waweze kuishi kama watu wengi ambao siyo walemavu.
 
Awali mkuu wa  chuo cha ufundi na marekebisho kwa watu wenye ulemavu cha sabasaba Bi. Fatuma Malenga ameiomba serekali kuangali uwezekano wa kukijengea uzio chuo na kuweka  vivuko maalumu pamoja na alama katika barabara ambayo ipo karibu na chuo ili kuwawezesha wenye ulemavu wa ngozi na walemavu wengine kuishi katika mazigira salama.
Share To:
Magpress

MagPress

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

0 comments so far,add yours