Kambi ya upinzani bungeni imeijua juu serikali kwa kitendo chake cha kushinikiza na kutumia ubabe wa kupitisha sheria ambazo ni kandamizi na zenye kubinya na kua uhuru wa vyombo vya habari hatua ambayo imesema inalenga kuliingiza taifa katika giza na kuondoa kabisa dhana ya uwazi ambayo serikali inaihubiri kila mara.
Akisoma hotuba ya kambi ya upinzani bungeni katika wizara ya habari utamaduni na michezo Mh Joseph Mbilinyi amesema inashangaza kuona kuwa inataka kujiingiza katika mgogoro waandishi wa habari bila ya kuwa na sababu yoyote ya msingi.
 
Aidha kambi ya upinzani imelaani kitendo cha kuwepo kwa vitisho vya kutaka kuuwawa kwa mmiliki wa kituo cha ITV Dk Reginalid Mengi kwa madai kuwa kituo chake kimekuwa kikitoa habari za uchochezi.
 
Awali akiwasilisha bajeti ya wizara ya habari utamaduni na michezo Mh Dk Fenella Mukangara amesema wizara yake itawasilisha muswada wa sheria ya huduma za habari ambapo ukipita utasaidia kuweka misingi imara katika sekta ya habari.
 
Lazaro Nyalandu ni waziri wa maliasili na utalii ambaye naye amewasilisha bajeti yake nakubainisha mipango mbalimbali yakiwemo   namna ya kupambana na ujangili.
 
Kwa upande waziri kivuli wa wizara hiyo mchungaji Peter Msigwa ameitaka serikali kuteketeza shehena ya pembe za ndovu ambazo imezikamata ili kuipunguzia serikali mzigo wa gharama wa kutunza pembe hizo.
Share To:
Magpress

MagPress

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

0 comments so far,add yours