Wananchi wilayani Simanjiro mkoani Manyara wameiomba serikali kutumia fedha zinazookolewa na Mh rais Dr John Magufuli kwa kuziba mianya ya matumizi mabaya na yasiyo ya lazima kusaidia kupunguza makali ya tatizo la ukosefu wa huduma za afya katika maeneo yenye mazingira magumu yakiwemo ya wilaya hiyo.  
Wakizungumzia tatizo la uhaba wa vitendeakazi unaovikabili vituo vya afya katika wilaya hiyo wananchi hao wamesema pamoja na changamoto katika sekta ya afya kuwa tatizo la kitaifa baadhi ya maneneo yakiwemo ya wilaya ya Simanjiro ni kubwa zaidi na yanahitaji kupewa kipaumbele ama upendeleo maalumu.
Aidha wametaja baadhi ya changamoto zinazovikali vituo vya afya katika wilaya hiyo kuwa ni pamoja na uhaba wa vitendeakazi, watumishi na ukosefu wa mahitaji ya damu ambayo ni makubwa zaidi kwa wanawake wanapokwenda kujifungua na watu wanaopatwa na majanga mbalimbali  ya ajali.
Msaidizi wa mganga mkuu wa kituo cha afya cha Mererani Dr. Kasian Mbwambo amewashukuru baadhi ya wasamaria wanaojitolea kwa hali na mali kusaidia kupunguza makali ya matatizo yaliyopo wakiwemo vijana waliojitolea damu kwa ajili ya wenzao wenye mahitaji.
Simanjiro ni miongoni mwa wilaya za mkoa wa Manyara ambazo  asilimia kubwa ya wananchi wake ni wafugaji ambao wakikabiliwa na  tatizo la ukosefu wa huduma bora za afya kwa muda mrefu sasa.

Share To:
Magpress

MagPress

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

0 comments so far,add yours