Mfanyabiashara wa Tanzania Bw. Patrick Ngowi ni miongoni mwa wafanyabiashara 100 walioingia fainali za kuwania tuzo ya mfanyabiashara bora kijana wa mwaka barani afrika, zitakazofanyika Afrika kusini novemba 14 mwaka huu.

Akiwa na umri wa miaka 28, Bw. Patrick Ngowi ambaye ni mwenyekiti wa kampuni ya Helvetic Group, inayotengeneza vifaa vya umeme wa jua, ametangazwa kuwa ni miongoni mwa wafanyabiashara 100 walio na umri usiozidi miaka 40, waliofanikiwa na wanaotarajiwa kufanya vizuri zaidi miaka ijayo.
 
Katika orodha hiyo wapo watanzania wengine 9, ikiashiria kuwa kuna uwezekano kuwa asilimia 10 ya wafanyabiashara wakubwa wa miaka ijayo barani Afrika, watakuwa ni watanzania.
 
Kwa mujibu wa rais wa taasisi ya Choiseul Bw. Pascal Larot, kila mwaka taasisi yake hufanya utafiti wa kusaka na kuorodhesha katika madaraja wafanyabiashara vijana wanaochipukia kiuchumi, wenye umri usiozidi miaka 40, ambao watashiriki kikamilifu katika kujenga uchumi wa bara hili miaka ya hivi karibuni.
 
Hivi karibuni chaneli ya televisheni ya mambo ya fedha na biashara - CNBC ilimtunuku Bw. Patrick Ngowi tuzo ya mwaka ya mfanyabiashara kijana wa Afrika Mashariki, katika hafla iliyofanyika jijini nairobi, kenya, ambayo mwenyekiti mtendaji wa IPP Dr Reginald Mengi pia alitunukiwa  tuzo ya mfanyabiashara bora wa mwaka Afrika Mashariki.
Share To:
Magpress

MagPress

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

0 comments so far,add yours