Whatsapp yawakaba koo “waongo”
11 hours ago
Kuanzia leo longo longo ya kwamba sikuupata ujumbe wako
wa WhatsApp itakuwa historia, au kudai kuwa ujumbe
haujafika utakuwa unaongopa mchana kweupe.
Huduma hiyo inapatikana kupitia Whatsapp katika simu
zote za mkononi zenye uwezo wa kuitumia
Tick ya kijivu ina maana kuwa ujumbe umetumwa, tick
mbili za kijivu zina maana ujumbe umemfikia mlengwa,
na tick mbili za blue zina maana kuwa mlengwa
ameusoma ujumbe uliotumwa
Ukibonyeza na kushikilia ujumbe uliotuma inatokea
Pressing and holding an individual message shows the
Message Info option
Ukibofya utaona muda kamili ambao ujumbe huo ulisomwa
Maoni kuhusu mabadiliko hayo yamepokelewa tofauti
katika mitandao ya kijamii, wapo ambao
hawajafurahishwa
Whatsapp haijatoa sababu za kufanya mabadiliko hayo
ambayo yamewakera baadhi ya watumiaji.
Kuanzia jana huduma hiyo inayomilikiwa na Facebook-
itakuwa ikionyesha tick mbili za rangi ya blue upande wa
chini kulia katika kila ujumbe unaotuma kubainisha kuwa
umesomwa.
Na ukibofya ujumbe wenyewe utaona muda kamili ambao
mlengwa alifungua na kuusoma ujumbe husika.

Share To:
Magpress

MagPress

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

0 comments so far,add yours