Wakazi wa nyumba zaidi ya mia moja na hamsini zilizokamilika na zilizo katika ujenzi kwenye eneo la vikongoro -CHANIKA wamejikuta wakipoteza makazi yao baada ya nyumba hizo kuvunjwa na serikali wilaya ya ilala kwa kudaiwa kuwa ni wavamizi.
Ni sehemu ya wakazi wa eneo hilo la vikongoro wakipaza sauti zao mara baada ya ITV kufika eneo la tukio kushuhudia kilichotendeka ambapo wakazi hao wamesema wamevunjiwa nyumba  zao pamoja na zile walizokuwa wakiendelea kujenga ilhali wanamiliki maeneo hayo kihalali.
 
Mmoja kati ya wakazi  wa eneo hilo EFESO MSEMO amesema vijana waliohusika na kufanya  uvunjaji huo walikuwa wakichukua  vitu walivyokuwa wakikuta ndani ya nyumba hizo sambamba na kunywa vinywaji walivyokuwa wakikuta katika maduka wanayoyavunja.
 
Mwenyekiti wa serikali  ya mtaa huo ameiambia ITV kwa njia ya simu kuwa alipewa taarifa na kamanda wa polisi wa wilaya ya kipolisi ya ukonga kuwa uvunjaji huo unatokana na wakazi hao kuvamia katika eneo ambalo linamilikiwa kihalali na mtu mwingine.
Share To:
Magpress

MagPress

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

0 comments so far,add yours